FIDA yamchemkia Magoha kuhusu dhulma shuleni

0

Muungano wa wanawake mawakili FIDA umetofautiana na waziri wa Elimu Profesa George Magoha kuhusiana na visa vya dhulma za kimapenzi shuleni.

Mwenyekiti wa FIDA Nancy Ikinu anasema onyo la waziri Magoha kwa wasichana wa shule kutokubali kutongozwa na walimu wao si suluhu kwa visa hivyo.

Badala yake, Ikinu anasema sheria inamlinda msichana wa kike kwa kuharamisha mahusiano ya kiampenzi na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane.

FIDA imeitaka wizara ya Elimu kuweka mwongozo wa kuwalinda watoto dhidi ya kudhulumiwa kimapenzi shuleni na pia kutoa adhabu kali kwa walimu ambao wanawadhulumu watoto.

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2019, Kenya ni taifa la tatu duniani kwa kuwa na wanafunzi wengi wajawazit duniani huku shule zikiwa za pili katika kuwadhulumu watoto wa kike.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here