Wagonjwa 10 zaidi wamefariki kutokana na ugonjwa wa corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya maafa nchini kuwa 634.
Katibu mkuu wa wizara ya afya Dkt. Mercy Mwangangi anasema watu wengine 121 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 23,364.
Idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini imeongezeka na kufikia 36,301 baada ya watu 96 kupatikana na virusi hivyo wakiwemo wanaume 70 na wanawake 26.
Msambao wa visa hivyo ni kama ifwatavyo; Nairobi 26, Kisii 10 , Busia 8, Mombasa, Kisumu na Uasin Gishu 7, Machakos 6, Kericho 5, Kilifi 4, Kiambu, Samburu, Kajiado, Kiambu na Nakuru 2, Kakamega, Embu, Makueni Taitataveta, Meru, Narok na Bomet 1.