Kaunti kupewa pesa zaidi aahidi rais Kenyatta baada ya kukutana na Odinga

0

Serikali za kaunti zitaongezewa Sh50b zaidi katika kipindi kijacho cha matumizi ya pesa kufuatia mkutano baina ya rais Uhuru Kenyatta, kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga na mwenyekiti wa baraza la magavana Wycliffe Oparanya.

Kufuatia hilo, rais Kenyatta aliyekutana na viongozi hao katika Ikulu ya rais Nairobi amewataka maseneta kutanzua mgogoro uliopo kuhusu mgao wa fedha ili kuepuka mgogoro wa kifedha katika serikali za kaunti.

Kiongozi wa walio wengi Samwel Poghisio, naibu wake Fatuma Dullo, kiraja wa wengi Irungu Kangata na naibu wake Farhiya Haji walihudhuria mkutano huo katika ikulu ya rais Nairobi.

Ikumbukwe kwamba maseneta zaidi ya mara moja wameshindwa kuelewana kuhusu mswada huo hali ambayo imewafanya magavana kutishia kufunga kaunti kuanzia Alhamisi wiki hii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here