Corona imeua walimu 15 yasema TSC

0

Takriban walimu 15 wa shule za msingi wameaga dunia kutokana na virusi vya corona.

Kulingana na afisa mkuu mtendaji wa tume ya walimu nchini (TSC) Nancy Macharia, walimu hawo ni pamoja na walimu wakuu 8 ambao walipoteza maisha yao wakiendelea na shughuli zao za kuwahudumia wanafunzi.

Wakati uo huo rais Uhuru Kenyatta ameamuru walimu wote kote nchini kupata chanjo dhidi ya virusi vya corona pasipo kuzingatia umri wao.

Wakati huo uo Macharia amesema tume hiyo itawazawadi walimu ambao wataandikisha matokeo bora pamoja na wale ambao walifanya jitihada katika kuhakikisha mitihani ya darasa la nane (KCPE) inendelea na kukamilika.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here