Bunge la kitaifa limeanza kibarua cha kuwasaili makamishna wanne wateule wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini (IEBC).
Juliana Cherera amekuwa wa kwanza kufika mbele ya kamati ya bunge hilo kuhusu haki na masuala ya sheria (JLAC) inayoongozwa na mbunge wa Kigumo Muturi Kigano kuhojiwa.
Kamati hiyo pia imemuhoji Francis Wanderi ambaye amejitetea akisema ana uwezo wa kuleta uongozi unaostahili katika tume hiyo ya uchaguzi.
Makamishna wengine ni; Irine Masit na Justus Nyang’aya walioteulia na rais Uhuru Kenyatta mapema mwezi huu.
Wanne hao walipendekezwa na rais baada ya kuhojiwa na jopo lilililoongozwa na Elizabeth Muli
Nafasi hizo za IEBC zilisalia wazi kufuatia kujiuzulu kwa Roselyne Akombe, Connie Maina, Margret Mwachanya na Paul Kurgat.