Uhuru amsimamisha kazi jaji Mary Muthoni Gitumbi

0

Rais Uhuru Kenyatta amemsimamisha kazi Jaji wa Mahakama ya Mazingira Mary Muthoni Gitumbi kwa misingi ya kutokuwa katika hali nzuri kiakili.

Kwenye notisi iliyochapishwa katika gazeti rasmi la serikali Agosti 23, rais Kenyatta amebuni jopo litakaloangazia misingi ya kumuondoa jaji huyo.

Tume ya huduma za mahakama (JSC) ilipendekea kutimuliwa kwa jaji huyo kwa kuzingatia rekodi zake matibabu zilizoonesha kuwa hayuko katika hali nzuri kiakili kutekeleza majukumu yake.

Jopo hilo litaongozwa na Jaji Hellen Omondi wanachama wakiwa majaji; Luka Kimaru, Linnet Ndolo, Peter Murage, Mary Bonyo, Dr. Frank Njenga, na Dr. Margaret Makonyengo.

Makatibu wenza wa jopo hilo ni Josiah Musili na Dr. Patrick Amoth huku mawakili wakiwa Emmanuel Bitta na Peter Njeru.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here