Bunge la kaunti ya Kisii limekuwa la NANE kupitisha mswada wa marekebisho ya katiba BBI.
Kaimu spika wa bunge hilo Amos Onderi anasema uamuzi wa kupitisha mswada huo uliafikiwa kwa kauli moja.
Gavana wa kaunti hiyo ya Kisii James Ongwae amelipongeza bunge la kaunti hiyo kwa kupitisha mswada huo.
Kisii inajiunga na Kajiado, Trans Nzoia, Pokot Magharibi, Busia, Homa Bay, Kisumu na Siaya kupitisha mswada huo.
Hii inamaanisha kwamba mswada huo unahitaji kuungwa mkono na kaunti 16 pekee ili kuwasilishwa bungeni na kisha kura ya maamuzi.
Bunge la kaunti ya Baringo ndilo la kipekee kupinga mswada huo kufikia sasa.
Mswada huo unahitaji kuungwa mkono na mabunge ya kaunti yapatayo 24 kati ya 47 ili kufanikisha mabadiliko ya sheria.









