Mali ya thamani ya pesa isiyojulikana imeteketea baada ya moto mkubwa kuteketeza afisi za bunge la kaunti ya Kisii.
Chanzo cha moto huo uliozuka mapema leo hakijabainika na tayari maafisa wa polisi wamenzisha uchunguzi huku stakabadhi muhimu zikiripotiwa kuchomeka.
Gavana wa Kisii James Ongwae aliyezuru eneo hilo amewataka maafisa wa polsii kuharakisha uchunguzi ili kubaini iwapo moto huo ulianzishwa kimaksudi.
Inaripotiwa kuwa moto huo ulilenga mahali ambapo vikao vya bunge la kaunti hufanyika.
Spika wa kaunti hiyo David Kombo anasema kisa hicho kinasikitisha kwani nguvu za umeme zilikuwa zimekatwa kuruhusu ukarabati.









