Watu 415 wapona baada ya kuambukizwa Corona

0

Idadi ya watu waliopona baada ya kuambukizwa virusi vya corona nchini imepita elfu ishirini na moja baada ya watu 415 kupona kwa muda wa saa ishirini na nne zilizopita.

Akizungumza katika kaunti ya Bomet, katibu mkuu katika wizara ya afya Rashid Aman anasema miongoni mwa wlaiopona leo, 161 wamekuwa wakipokea matibabu nyumbani na wengine 254 kutoka hospitati mbalimbali nchini na kufikisha idadi ya waliopona nchini kuwa 21,059.

Watu 179 wamepatikana na virusi vya corona baada ya sampuli 4,178 kupimwa na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa na 34,884.

Msambao wa virusi hivyo katika kaunti ni kama ifuatavyo; Nairobi 66,Garrisa 21, Turkana na Nakuru 12 ,Busia 11, Taitataveta 10,  Kiambu 9,Kitui 6, Kajiado, Transnzoia na Nyamira 3, Kisii 2, Muranga, Nyamira, Meru 1.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here