Idadi ya visa vya ugonjwa wa corona nchini inaendelea kupungua huku Kenya ikiandikisha visa 83 pekee katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita baada ya kupima sampuli 3,093.
Wizara ya afya inasema hii inafikisha 35,103 idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini kufikia sasa.
Msambao wa visa hivyo ni kama ifwatavyo; Narobi (27), Busia (15), Kisumu (12), Nakuru & Machakos (7), Kiambu (5), Laikipia & Kisii (3), Kirinyaga, Mombasa, Nyandarua & Uasin Gishu (1).
Watu 72 wamepona na kufikisha idadi ya waliopona ugonjwa huo kuwa 21,230 huku idadi ya maafa ikifikia 597 baada ya kufariki kwa wagonjwa watatu zaidi.