Zaidi ya Maafisa wa Polisi 1,000 Watumwa Kulinda Uchaguzi wa Ol Kalou.

0

Inspekta Jenerali wa Polisi, Douglas Kanja, amesema zaidi ya maafisa 1,000 wa Polisi wametumwa kuhakikisha uchaguzi mdogo wa ubunge wa Ol Kalou unafanyika kwa amani.

Akizungumza Jumanne Tarehe 14 Julai 2026, wakati wa kikao cha Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuhusu maandalizi ya uchaguzi huo, Kanja amesema vituo vyote 114 vya kupigia kura vitakuwa na ulinzi wa kutosha kulingana na taratibu za idara ya polisi.

“Hii ina maana kwamba tumewapeleka angalau maafisa wawili wa polisi katika kila kituo cha kupigia kura. Jukumu lao ni kulinda vifaa vya uchaguzi na mchakato mzima wa upigaji kura, kutoa usalama wa kutosha na kuhakikisha maafisa wa uchaguzi wanatekeleza majukumu yao bila vikwazo.”

“Aidha, katika kila kituo cha kupigia kura kuna timu ya maafisa wasiopungua 14 ili kuhakikisha usalama umeimarishwa ipasavyo,” amesema Kanja.

Ameongeza kuwa kila kituo kitakuwa na angalau maafisa wawili wa polisi watakaolinda vifaa vya uchaguzi, kusimamia usalama wa mchakato wa upigaji kura na kuhakikisha maafisa wa uchaguzi wanatekeleza majukumu yao bila vikwazo.

“Nimetuma vikosi vinne vya maafisa wa GSU, vikosi vinne vya Kitengo cha Kuzuia Wizi wa Mifugo ASTU, Pia tumewapeleka maafisa wa kutosha kutoka Idara ya Upelelezi wa makosa ya Jinai (DCI), ambao jukumu lao litakuwa kukusanya taarifa za kijasusi, kufanya uchunguzi, kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watu au makundi yatakayohusika na ukiukaji wowote wa sheria za uchaguzi,”

“Kama Inspekta Jenerali wa Huduma ya Kitaifa ya Polisi, ninawahakikishia wakazi wa Ol Kalou kwamba watatekeleza haki yao ya kidemokrasia katika mazingira ya uchaguzi huru, wa haki, wenye amani na usalama, kwa kuzingatia Katiba na sheria za nchi.” ameongeza Kanja.

Aidha, DCI imepewa jukumu la kukusanya taarifa za kijasusi, kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria watu watakaobainika kujihusisha na ukiukaji wa sheria za uchaguzi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here