Takriban wahudumu wa afya 4,698 wameambukizwa virusi vya corona nchini kufikia sasa.
Wizara ya afya inasema idadi hiyo inajumuisha wanawake 2,562 na wanaume 2,136.
Idadi ya waliofariki kutokana na makali ya ugonjwa huo inasalia kuwa 38.
Kufikia sasa watu 721,509 wamepewa chanjo dhidi ya ugonjwa huo wa corona wakiwemo wahudumu wa afya wapatao 143,050.
Nairobi ingalia inaongoza kwa kutoa chanjo hiyo kwa watu 229,385 ikifuatiwa na Nakuru ambayo imechanja watu 43,590, Uasin Gishu (36,576), Kiambu (35,711) huku Nyeri ikifunga tano bora kwa kuwachanja watu 25,977.
Kaunti zilizo na idadi ndogo ya watu waliopata chanjo hiyo ni Marsabit (470), Lamu (537), Tana River (680) na Isiolo (1,392).