Wizara ya afya nchini Uganda imewaagiza wahudumu wa afya nchini kuvalia barakoa mbili wanapokuwa kazini ndio wasiambukizwe ugonjwa wa corona.
Katika taarifa, mkurugenzi wa shughuli za matibabu Dr. Henry Mwebesa amesema kisayansi, imebainika kwamba kuvalia barakoa mbili kuna uwezo wa kuzuia corona ikizingatiwa kwamba wahudumu wa afya wako katika hatari ya kuambukizwa.
Wizara hiyo vile vle imewaagiza wahudumu wa afya kuzingatia kikamilifu muongozo wa kuzuia msambao wa ugonjwa huo wanapokuwa kazini.
Agizo hili linajiri wakati ambapo taifa hilo la Afrika Mashariki linashuhudiwa wimbi la pili la maambukizi ya corona.