Wezi wavunja kanisa Lurambi na kuiba nguo za pasta

0

Waumini wa kanisa la Makutano PAG, kule Lurambi kaunti ya Kakamega wanakadiria hasara baada ya wezi kuvunja kanisa lao na kuiba mali ya thamani isyojulikana.

Wakiongozwa na mama Prisca Orembo, waumini hao wanasema walifika kanisani jana kama kawaida kwa ibada ila wakapigwa na butwaa kugundua kanisa lao lilikuwa limevunjwa.

Wezi hao pia wanaripotiwa kuvunja nyumba ya mchungaji wa kanisa hilo na kuiba bidhaa za nyumba ikiwemo mtungi wa gesi wa kupika, chakula na hata nguo ikiwemo suti, nguo za ndani za mchungaji na pia viatu.

Waumini hao sasa wanatoa wito kwa polisi kufanya uchunguzi wa kina na kuwanasa waliohusika

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here