Evans Karani, mshukiwa wa mauaji ya mpenziwe Catherine Nyokabi mwenye umri wa miaka Ishirini na mitano atasalia rumande kwa siku kumi na nne zaidi kuwapa muda wa kukamilisha uchunguzi.
Mshukiwa amefikishwa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Thika Oscar Wanyaga kwa njia ya kimtandao kutoka katika kituo cha Polisi cha Juja anakozuiliwa.
Karani ambaye awali aliwaambia Polisi kwamba hajutii kumuua Nyokabi ambaye amekuwa mpenziwe kwa muda wa miaka miwili amemuomba hakimu huyo kuharakisha hukumu dhidi yake.
Kesi hiyo inatarajiwa kutajwa tena tarehe tatu mwezi ujao.
Mwili wa marehemu ulipatwa kwenye gari la mshukiwa wikendi iliyopita baada ya kukwama matopeni alipokuwa anajaribu kuutupa baada ya kumuua.