Wendani wa Ruto wamkaanga Uhuru kwa kuwatishia majaji

0

Wendani wa naibu rais William Ruto wameendelea kumkaanga rais Uhuru Kenyatta kutokana na kile wametaja kama kuwatishia majaji kufuatia uamuzi wao wa kusitisha mchakato wa kurekebisha katiba kupitia BBI.

Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen kupitia mtandao wake wa Twitter amesema hatua ya rais kuwatishia majaji haileti heshima kwa taifa hili wala afisi ya rais.

Kwa upande wake, mbunge wa Nyali Mohammed Ali amemkosoa rais Kenyatta kwa kuwasomea majaji wakati wa sherehe za kitaifa.

Jicho Pevu anavyofahamika na wengi amesema kuwatishia majaji kwa kusimamisha mchakato wa BBI ni kuingilia uhuru wa idara ya mahakama.

Amesema hiyo sio suluhu kwa matatizo yanayowakumba Wakenya huku akitaka katiba kuheshimiwa.

Akirejelea uamuzi wa mahakama kuu uliosimamisha mchakato wa kurekebisha katiba kupitia BBI, rais amedokeza kwamba mahakama ilikosa kuzingatia kikamilifu umuhimu wa mchakato huo na uamuzi wa Wakenya wengi wanaotaka katiba kubadlishwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here