Waiguru anusa shida kwa Jubilee

0

Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru amekuwa kiongozi wa hivi punde kuitisha mabadiliko ya uongozi katika chama tawala cha Jubilee kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, tunamnukuu Waiguru akisema kwamba ‘mvua imetunyeshea na matarajio yetu yanadidimia. Umewadia wakati wa kujiangalia upya’.

Ameongeza kuwa chama cha Jubilee kinabeba maono ya Wakenya wengi na kwamba kilibuniwa kwa nguvu za wengi.

Na huku uchaguzi mkuu ukikaribia, Waiguru amesema kwa sasa chama hicho kinafaa kuwa na mfumo tofauti kinyume na uliokuwa miaka 10 iliyopita.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here