Watu 150 zaidi wakutwa na corona

0

Watu 150 wamekutwa na virusi vya corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita baada ya kupima sampuli 3,117 na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 101,159.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe ametangaza kuwa watu 70 wamepona virusi hivyo na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 84,060.

Idadi ya maafa imeongezeka na kufikia 1, 769 baada ya wagonjwa 3 zaidi kufariki.

Wagonjwa 459 wamelazwa katika hospitali mbalimbali 26 wako katika vyumba vya wagonjwa mahututi 11 wanasaidiwa na mashine kupumua.

Nairobi inaongoza na visa 101, Uasin Gishu 9, Garissa 6, Mombasa 5, Kajiado 4, Machakos, Meru, Siaya, Kisumu, Migori, Taita Taveta, Kilifi, Kiambu, Nakuru na Kitui 2.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here