Wanaopania kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu wa 2022 wataruhusiwa kutumia hadi Sh4.4b kwenye kampeini imesema tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC.
IEBC chini ya uenyekiti wake Wafula Chebukati imetoa mwongozo wa pesa zitakazotumika na wawaniaji wote ikiwemo urais, magavana, maseneta, wabunge na wawakilishi wadi kuambatana na mswada wa fedha za kampeini.
Vyama vya kisiasa vitaruhusiwa kutumia hadi Sh17.7b kwenye kampeini.
Muwaniaji wa gavana kaunti ya Turkana ndiye atatumia kiasi kikubwa cha pesa IEBC ikiweka kiwango cha hadi Sh123M huku Nairobi ikiwa Sh117M.
Tume hiyo inasisitiza kuwa uchaguzi huo mkuu ni sharti uandaliwe Agosti 9,2021 sawa sawa na ilivyoratibiwa kwenye katiba.









