Mwanamke mmoja ni miongoni mwa washukiwa wanne walioshtakiwa leo kwa kumuibia marehemu.
Kwenye kosa la kwanza, washukiwa Muguna Mutembei na Eugene Shivachi wameshtakiwa kwa makosa 12 ya kuiba Sh2.2M kutoka kwa Amos Ngata Muiruri ambaye alikufa.
Inadaiwa kuwa washukiwa hao waliiba pesa hizo kutoka akaunti za KCB, Equity na NCBA zinazomilikiwa na marehemu.
Mahakama imewaachiliwa kwa dhamana ya Sh500,000 kila mmoja.
Katika kosa la pili, wawili hao wameshtakiwa pamoja na wenzao Morris Riungu na Jane Gathogo kwa kuwaibia watu waliokufa kwa kutumia laini tofauti tofauti za simu.
Mahakama imewaachiliwa kwa dhamana ya Sh200,000 kila mmoja.
Genge hilo limekuwa likitumia magazeti ya kila siku nchini kufahamu haswa matajiri wanaofariki na kutumia muda wa maombolezo kwa familia kuibia wapendwa wao ambao wamefariki.
Katika taarifa, idara ya upelelezi nchini DCI inasema washukiwa wanatumia muda wa maombolezo kwani ndio wakati familia haiwezi kushuku kuna wizi unaendelea.
DCI inasema wengine wanaolengwa kwenye wizi huo ni wakongwe na pia watu wanaosafiri kwenda ughaibuni, na haswa matajiri.









