Wakurugenzi wa hospitali ya Mama Lucy kuendelea kuzuiliwa kuhusu sakata ya watoto

0

Afisa mkuu mtendaji wa hospitali ya Mama Lucy Emma Mutio na wahudumu wengine wawili wa Afya watasalia rumande kwa siku mbili zaidi kuruhusu uchunguzi wa madai ya wizi wa watoto.

Hakimu mkuu wa mahakama ya Milimani Bernard Ochoi ameagiza Mutio na washukiwa wenza Fred Leparan na Reginah Musembi waendelee kuzuiliwa kwa misingi kwamba wakiachiliwa huenda wakahitilafiana na ushahidi kwenye kesi hiyo.

Katika ufichuzi uliofanywa na shirika la habari la BBC, inadaiwa kuwa watatu hao wamekuwa wakishirikiana na washukiwa wengine kuiba watoto na kisha kuwauza kwa kati ya shilingi 70,000-300,000.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here