Wahudumu wa afya katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta wameanza mgomo wao kualamikia nyongeza ya mishahara waliyofaa kupewa baada ya hadhi ya hospitali hiyo kupandishwa.
Wakiongozwa na katibu mkuu wa muungano wa wauguzi (KNUN) Seth Panyako wahudumu hao wa afya ambao wamesabbaisha kusambaratika kwa huduma za matibabu wanaishtumu tume ya kutathmini mishahara ya watumishi wa umma SRC kwa kupinga nyongeza ya mishahara yao.
Wafanyikazi hao ikiwemo madaktari na wauguzi wanasema hawatarejea kazini iwapo mishahara yao haitaongezwa.
Misururu ya mikutano iliandaliwa jana, Jumapili, kujaribu kutafuta suluhu lakini hadi kufikia sasa hakuna makubaliano yoyote yameafikiwa huku SRC ikishikilia kuwa hatua ya kupandisha hospitali daraja haikumaanisha mishahara pia itaongezwa









