Shule za chekechea kufunguliwa baada ya zile za msingi na secondari wasema CoG

0

Shule za chekechea zitafunguliwa mwezi mmoja baada ya kufunguliwa kwa shule za msingi na zile za upili.

Baraza la magavana kupitia kwa mwenyekiti wake Wycliffe Oparanya linasema hili litawezesha taifa kufuatilia kwa karibu hali ya msambao wa virusi vya corona kabla ya kuwaruhusu watoto wadogo kuripoti shuleni.

Kutokana na hilo baraza hilo linaitaka serikali kuu kuzipa kaunti vifaa vya kupima watoto ili kuwahakikishia usalama wao wanaporejelea masomo.

Baraza hilo vile vile limesema litashauriana na mawakili wake kuhusu ushauri wa kulivunja bunge kabla ya kutoa kauli ya pamoja.

Haya yanajiri siku moja baada ya mahakama kusitisha utekelezwa wa ushauri huo uliotolewa kwa rais Uhuru Kenyatta na jaji mkuu David Maraga hadi kesi iliyowasilishwa mahakamani isikilzwe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here