Bunge la kitaifa limetumia kikao maalum cha Jumatano asubuhi kumuomboleza mwenzao wa Kiambaa Paul Koinange aliyefariki kutokana na matatizo yanayoambatana na corona.
Wabunge wamemtaja Koinange kama kiongozi mcha Mungu, shupavu na aliyekuwa tayari kutoa msaada alipohitajika.
Koinange alifariki mwishoni mwa mwezi jana katika hospitali ya Nairobi alipokuwa amelazwa baada ya kudhibitishwa kuwa na virusi vya corona.
Hadi kifo chake, Koinange alikuwa mwenyekiti wa kamati ya bunge la kitaifa kuhusu Usalama.
Tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imeratibu uchaguzi mdogo wa Kiambaa kuandaliwa Julai 15 mwaka huu.