Wabunge wa Kisumu walaumu MoH kufuatia kuingia kwa corona kutoka India

0

Baadhi ya wabunge kutoka Nyanza wameilaumu wizara ya afya kufuatia kuingia Kisumu kwa virusi vya corona vinayosababisha maafa nchini India.

Wabunge hao wakiongozwa na Olago Aluoch wa Kisumu Magharibi wanasema serikali ilipaswa kufanya mengi kuhakikisha kuwa virusi hivyo haviingii nchini na kutaka mikakati kabambe kuwekwa kuzuia msambao wake katika maeneo mengine.

Yakijiri hayo

Maambukizi ya ugonjwa wa nchini corona yako katika asilimia 8% baada ya watu 705 kupatikana nao katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Hii ni baada ya kupima sampuli 8,853 na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 162,098.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe katika taarifa, ametangaza kuwa watu 711 zaidi wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliopona nchini kuwa 110,480 huku maafa 25 zaidi yakidhibitishwa na kufikisha idadi hiyo kuwa 2,850.

Kuhusu shughuli ya utoaji chanjo ya Astrazeneca inayoendelea kote nchini, waziri Kagwe ametangaza kuwa jumla ya watu 906, 746  wamepata chanjo hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here