Visa vya dhulma za kimapenzi vyaongezeka wasema utafiti

0

Visa vya  dhulma za kimapenzi viliongezeka kwa asilimia tisini na mbili (92%) kati ya mwezi Januari na Juni mwaka jana.

Haya ni kulingana na utafiti uliofanywa na kituo cha uhalifu wa kitaifa ambao umetaja kaunti za Nairobi, Kakamega, Kisumu, Nakuru na Kiambu kama zinaongoza kwa kurekodi idadi kubwa ya visa hivyo.

Akitangaza matokeo ya utafiti huo, waziri wa jinsia Profesa Margaret Kobia ametaja unywaji wa pombe, utumizi wa dawa za kulevya, kuzorota kwa maadili, mizozo ya kinyumbani na malezi hafifu kama baadhi ya sababu zinazochangia kuongezeka kwa visa hivyo.

Waziri Kobia anasema jumla ya visa 5,009 viliripotiwa kati ya Januari na Disemba mwaka 2020 kupitia nambari ya dharura 1195.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here