Profesa Dr. Moni Wekesa ajitetea mbele ya JSC

0

Profesa Dr. Dr. Moni Wekesa amenadi sera zake kwa tume ya huduma za mahakama (JSC) akielezea ni kwa nini anatosha kuwa Jaji Mkuu wa Kenya.

Msomi huyo wa maswala ya kisheria ameahidi kuleta mabadiliko ikiwemo kumfanya mwananchi wa kawaida kuwa nguzo kuu katika mchakato wa kupatikana kwa haki kupitia kutoa hamasisho kwa umma kuhusu utendakazi wa idara ya mahakama.

Profesa Moni ameiambia JSC kwamba anajivunia kuwashawishi wanafunzi wa sheria katika vyuo vikuu vya Mount Kenya na Day Star kuvalia suti.

Kulingana na Profesa Moni, hakuna uhusiano wa karibu kati ya umma na idara ya mahakama na hivyo kuadhiri inavyoendesha huduma zake.

pWengine waliohojiwa kwa wadhifa huo ni pamoja na mawakili Fred Ngatia na Philip Murgor, majaji William Ouko, David Marete, Martha Koome, Juma Chitembwe na msomi wa maswala ya kisheria Profesa Kameri Mbote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here