Vigogo wa One Kenya Alliance wakutana

0

Vinara wa muungano wa One Kenya Alliance (OKA) wamefanya mkutano kushauriana kuhusu hatma ya gurudumu hilo la kisiasa.

Mkutano huo umehudhuriwa na Musalia Mudavadi (ANC), Kalonzo Musyoka (Wiper), Gideon Moi (KANU) na Moses Wetangula (FORD K).

Vigogo hao wa kisiasa wanasema lengo lao ni kuweka mikakati kuimarisha muungano wao ili ukubaliwe na Wakenya kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022.

Mkutano huo unawadia siku chache baada ya kuibuka hisia mseto kufuatia mkutano baina ya Gideon Moi, kinara wa chama cha ODM Raila Odinga na Muhoho Kenyatta nduguye rais Uhuru Kenyatta.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here