USHIRIKIANO WA KENYA, JAMHURI YA CONGO, JAMHURI YA AFRIKA YA KATI UTAIMARISHA USALAMA, BIASHARA

0
RUTO IN CONGO
RUTO IN CONGO

Kenya, Jamhuri ya Congo na Jamhuri ya Afrika ya Kati zitaungana katika vita dhidi ya ugaidi na ukosefu wa usalama barani Afrika.

Rais William Ruto alisema mataifa hayo matatu yamejitolea kuhakikisha kupatikana kwa amani na utulivu wa kudumu barani humo.

Alisema watashirikiana katika kupashana habari za kijasusi na kuchukua misimamo ya pamoja kwenye majukwaa ya kimataifa ili kukuza ajenda ya amani ya Afrika.

Kiongozi wa Nchi alisema nchi hizo pia zitakuwa na ushirikiano wa karibu katika kupambana na itikadi kali na vurugu kali za kivita ili kufikia amani, usalama na utulivu.

“Nchi zetu zinahitaji kufanya kazi pamoja ili kutafuta suluhu zinazofaa kwa matatizo ya pamoja yanayokabili amani na usalama wa kimataifa na kikanda,” alisema.

Rais Ruto aliyasema hayo siku ya Jumapili huko Oyo, Jamhuri ya Congo, wakati wa mkutano na marais Faustin-Archange Touadéra (Jamhuri ya Afrika ya Kati) na Denis Sassou Nguesso (Jamhuri ya Congo).

Viongozi hao walijitolea kuimarisha uhusiano baina ya mataifa hayo matatu na kukuza biashara ya ndani ya Afrika.

Rais Ruto alisema wanapania kuangalia kwa undani fursa za kibiashara zinazoibukia na ambazo hazijatumiwa kwa manufaa ya wananchi.

“Wakati umewadia wa Afrika kufanya biashara pamoja, na Kenya ina umakini katika kushirikiana na Jamhuri ya Afrika ya Kati na Jamhuri ya Congo ili kutimiza lengo hili zuri,” aliongeza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here