Ukame Wasababisha Uhaba wa Maziwa Nchini, Serikali Yasema.

0
Katibu wa Wizara ya Kilimo na Mifugo Jonathan Mueke

Serikali imezidi na kusisitiza ukame ndio chanzo kikuu cha uhaba wa maziwa ambao unaendelea kushuhudiwa nchini huku ikiashiria uwezekano wa bei ya maziwa kushuka mara tu mvua zitakaporejea.

Katibu wa Wizara ya Kilimo na Mifugo Jonathan Mueke, amesema hali ya ukame imeathiri uzalishaji wa maziwa, hali ambayo imechangia upungufu wa bidhaa hiyo katika soko.

Mueke amesema bei ya maziwa inatarajiwa kupungua mara tu mvua zitakaporejea na hali ya uzalishaji kurejea katika kiwango cha kawaida.

“Uzalishaji wa maziwa umeathiriwa na ukame; hiyo ndiyo sababu kuu ya uhaba wa maziwa.” Mueke ameeleza.

Licha ya changamoto ya ukame, Mueke amesema sekta ya maziwa nchini imeendelea kukua, huku uzalishaji ukiongezeka kutoka lita bilioni 4.6 hadi lita bilioni 5.5.

Kwa mujibu wa Mueke, ongezeko hilo limeifanya Kenya kuwa miongoni mwa wazalishaji wakuu wa maziwa barani Afrika.

“Katika sekta ya maziwa, tumekua, kutoka lita bilioni 4.6 hadi lita bilioni 5.5, jambo lililotufanya kuwa wazalishaji namba moja wa maziwa barani Afrika. Mauzo yetu ya nje yameongezeka karibu mara tatu.” Amesema Mueke.

Mueke pia amesema mauzo ya maziwa ya Kenya katika masoko ya nje yamekaribia kuongezeka mara tatu, akitaja hatua hiyo kama ishara ya ukuaji wa sekta ya maziwa nchini.

 

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here