Katika juhudi za kusaidia kupambana na ugaidi huko Mandera, Uingereza imeanzisha miradi inayolenga kutoa ajira kwa vijana wa eneo hilo ili kuwaepusha na kujiunga na makundi ya kigaidi.
Waziri wa mambo ya nje wa taifa hilo Jane Marriott amezuru kaunti hiyo Jumanne kuangazia mikakati ya kiuchumi iliyoanzishwa kwa makusudi ya kulifanya eneo hilo kuwa dhabiti.
Amesema Kenya na Uingereza wanashirikiana kuziwezesha jamii katika kaunti ya Mandera kujiendeleza kimaisha ili kukomesha uhasama baina yao na namna ya kutatua mizozo ibuka kwa amani.
Waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa na Gavana wa Mandera Ali Roba waliandamana na Jane Marriott kwenye ziara hiyo.