Uhuru kuelekea Ukambani mwishoni mwa Juni

0

Rais Uhuru Kenyatta anatazamiwa kuzuru eneo la Ukambani kwa siku mbili mwishoni mwa mwezi huu wa Juni.

Kwa mujibu wa ratiba, rais Kenyatta ambaye amekutana na viongozi kutoka Ukambani ameratibiwa kuzuru kaunti za Machakos na Makueni Juni 28 kabla ya kuelekea Kitui Juni 29.

Rais ametumia fursa hiyo kuwarai viongozi wote kushirikiana kuwahudumia wananchi badala ya kuendelea na siasa ambazo hazina mwisho.

Amesisitiza kwamba nia ya mchakato wa BBI ilikuwa ni kuliunganisha taifa na kuwa na umoja wa kitaifa.

Rais amesema malumbano ya kisiasa yanalirudisha taifa hili nyuma kimaendeleo kwa sababu ya siasa za kibinafsi.

Viongozi kutoka Ukambani wakiongozwa na Kalonzo Musyoka walifanya mazungumzo na rais katika Ikulu ya Nairobi kabla ya ziara hiyo.

Wengine waliokuwepo wakati wa mazungumzo hayo ya mashauriano ni magavana Charity Ngilu wa Kitui na Dkt. Alfred Mutua wa Machakos.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here