Uhuru azindua hospitali usiku

0

Rais Uhuru Kenyatta amezindua hospitali mpya tano katika kaunti ya Nairobi na kuziagiza kufanya kazi usiku na mchana.

Rais Kenyatta amezindua hospitali hizo ndogo Jumanne usiku katika juhudi za kupunguza msongamano wa watu wanaotafuta huduma za matibabu katika hospitali za Nairobi, Mbagathi na ile ya Pumwani.

 Rais Kenyatta aliyeandamana na mkurugenzi wa mamlaka ya NMS Mohamed Badi anasema aliamua kufanya uzinduzi huo majira ya usiku ili kuzingatia masharti ya kujikinga na virusi vya corona.

HospitaIi hizo zilizofunguliwa na Rais Kenyatta usiku ni hospitali za level ya pili mtaani Kangemi na Kawangware, pamoja pia ni hospitali za level ya tatu katika mitaa ya Mukuru Kwa Rueben, Tassia Kwa Ndege na Mukuru Kwa Njenga.

Rais Kenyatta amesema pia kuwa ametumia ziara hiyo ya usiku kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara katika mitaa ya mabanda Nairobi.

 

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here