Rais Uhuru Kenyatta amepigia debe mabadiliko ya katiba kupitia mchakato wa BBI kwenye ziara yake ya kikazi katika eneo la Pwani.
Rais Kenyatta akizungumza alipowapa wenyeji wa Rabai kaunti ya Kilifi hati miliki za ardhi zaidi ya alfu mbili amesema kupitia BBI, sauti ya kila Mkenya itasikika.
Rais aliyekuwa ameandamana na mawaziri Faridah Karoney (Ardhi), Mutahi Kagwe (Afya) na Fred Matiang’i (Usalama) amewarai wenyeji kutumia vyema vyeti hivyo kujinufaisha kimaisha badala ya kuuza.
Kiongozi wa taifa vile vile amezindua vifaa vya kupambana na ugonjwa wa Malaria vilivyotengenezwa humu nchini.
Vifaa hivyo vimetengenezwa na shirika la KEMRI kaunti ya Kilifi uzinduzi wake ukilenga kupiga jeki vita dhidi ya ugonjwa wa Malaria.