Kesho Ijumaa Juni 24 itakuwa ni siku kuu nchini Uganda kwa ajili ya maombi ya kitaifa taifa hilo likipambana na wimbi la pili la janga la corona.
Barua iliyotiwa sahihi na rais Yoweri Museveni imearifu kwamba siku hiyo itatumika kumuomba Mungu kuliokoa taifa hilo na janga hilo linaloendelea kusbabaisha maafa.
Maombi hayo yataandaliwa kwa njia ya mtandao mubashara kutoka Ikulu ya rais iliyoko Entebe kuanzia saa sita viongozi mbalimbali wa kidini wakitazamiwa kuhudhuria.
Mamilioni ya raia wa taifa hilo la Afrika Mashariki watafuatilia maombi hayo ya kumtafuta Mungu wakiwa nyumbani.