Tathmini: Nini kinafuata baada ya Joe Biden kushinda uchaguzi Marekani?

0

Wengi wanajiuliza, je nini kinafuatia baada ya Joe Biden na Kamala Harris kushinda uchaguzi wa urais nchini Marekani?

Licha ya kwamba rais wa sasa Donald Trump bado hajakubali kushindwa kwenye uchaguzi huo, inakadiriwa kuwa kizingiti kwa Biden na Harris ni kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi huo kutoka kwa Trump.

Wanaposubiri kuapishwa kwao Januari mwaka ujao, wawili hao watafahamu iwapo walichaguliwa kihalali kupitia kuhakikishwa kwa kura zilizopigwa katika kila jimbo.

Kimsingi, wawili hao wanastahili kuapishwa rasmi Januari 20, 2021 mjini Washingon, DC ilivyo kwenye katiba ya taifa hilo lenye ushawishi mkubwa duniani.

Kipindi hiki cha mpito, yaani baada ya uchaguzi na hadi kuapishwa kwake, rais mteule anaruhusiwa kuteua kundi litakaloongoza mpito wa mamlaka jambo ambalo tayari Biden amefanya.

Kundi hilo ndilo litateua baraza la mawaziri, kujadili maswala yatakayopewa kipau mbele na wajiandae kuongoza.

Katika safari hii ya kujiandaa kuliongoza taifa la Marekani, Biden na Harris ni sharti wawe na subira kwani Donald Trump hajakubali matokeo ya uchaguzi huo na mahakama ndio itabaini hatma ya hilo.

Ilivyo desturi za Marekani, anayeshindwa kwenye uchaguzi anapaswa kumpigia simu mshindi kukubali matokeo na kumpongeza ila mara hii mambo ni tofauti.

Wakati huu wote, Kamala Harris mwanamke wa kwanza kuchaguliwa makamu wa rais atakuwa anajifunza majukumu yake mapya huku akiwateua watu watakaomsaidia kuwajibikia majukumu yake.

Itakapofika Januari 20, ni yeye ndiye atakuwa wa kwanza kuapishwa kabla ya kumpisha Biden kila kiapo cha kuwa rais wa 46 wa Marekani.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here