Sonko kusalia kizimbani hadi wiki ijayo

0

Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko amepata pigo baada ya mahakama kuhairisha kutoa uamuzi wa ombi lake la kutaka kuachiliwa kwa dhamana.

Wakili wake Assah Nyakundi amewaambia wanahabari kuwa mahakama ya Kiambu imehairisha kutoa uamuzi wa ombi la mteja wake hadi Jumanne wiki ijayo.

Hii ina maana kuwa Sonko atazuiliwa kwa muda wa siku tano zaidi akisubiri uamuzi huo kutolewa.

Haya yanajiri huku mahakama ya Kahawa ikitarajiwa pia kutoa uamuzi wa ombi la upande wa mashtaka kutaka kumzuilia Sonko kwa siku thelathini zaidi, kukamilisha uchunguzi wa madai kuwa amekuwa akihami kundi lake la kigaidi, kwa lengo la kutekeleza mashambulizi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here