Shule ya wasichana ya Lugulu yafungwa baada ya madai ya ubakaji shuleni

0

Shule ya wasichana ya Lugulu kaunti ya Bungoma imefungwa kwa muda usiojulikana baada ya wanafunzi kuandamana kulalamikia madai ya ubakaji shuleni.

Bodi ya shule hiyo imechukua hatua hiyo ili kurejesha hali ya utulivu na kutoa nafasi ya uchunguzi kufanywa kubaini ukweli wa madai hayo.

Katibu mkuu wa muungano wa walimu kaunti hiyo Aggrey Namisi amesema wanafunzi hao wanadi pia kuwa wamekuwa wakinyanyaswa kinjinsia na kuripoti kwa malimu mkuu Dina Cheruiyot ambaye hajachukua hatua yeyote.

Wanafunzi hao waliandamana hadi katika kituo cha Polisi cha Webuye kushinikiza kukamatwa kwa jamaa anayedaiwa kuhuhusika.

Mwanafunzi huo anaarifiwa kubakwa Jumamosi asubuhi aliokuwa anaoga kabla ya kuelekea darasani.

Aliokolewa na mwenzake aliyefika kwa ghafla na kuanza kupiga kamsa na kumlazimu mshukiwa kutoroka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here