Hatma ya Gavana Mike Sonko kubainika juma lijalo

0

Gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko atafika mbele ya bunge la Senate kujitetea na wala sio mbele ya kamati ya maseneta 11 kama ilivyokuwa imependekezwa hapo awali.

Spika wa bunge la Senate Ken Lusaka amesema uamuzi huo umeafikiwa baada ya kiongzi wa walio wengi Samwel Poghisio kukosa kushughulikia notisi ambayo ingetoa mwongozo ambao ungefuatwa kuhusu kuchunguza madai dhidi ya Sonko.

Kutokana na hilo, bunge hilo litakuwa na vikao maalum tarehe kumi na saba na kumi na nane ambayo ni Alhamisi na Ijumaa wiki ijayo kumchunguza Sonko.

Waliokuwa wamependekezwa kwenye kamati hiyo ni maseneta Samson Cherargei (Nandi), Charles Kibiru (Kirinyaga), Hargura Godana (Marsabit), Abdullahi Ali (Wajir), Okongo Omogeni (Nyamira), Mohamed Faki (Mombasa) na Fred Outa (Kisumu).

Wengine ni maseneta wateule Alice Milgo, Christine Zawadi, Judith Pareno na Petronilla Were.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here