Wizara ya Afya imeagiza mamlaka ya kusambaza dawa na vifaa vingine vya matibabu nchini KEMSA kuanza kupeana vifaa wanavyohifadhi vya kujikinga na virusi vya corona kuanzia siku ya Ijumaa.
Akihojiwa na wanachama wa kamati ya bunge la seneti kuhsuu Afya chini ye uenyekiti wa seneta Michael Mbito, katibu mkuu katika wizara ya Afya Dr Mercy Mwangangi amesema wameagiza KEMSA kuuza vifaa hivyo kwa bei nafuu.
Hatua hiyo huenda ikawa afueni kwa wahudumu wa Afya ambao wamekuwa wakilalamikia ukosefu wa magwanda ya kujikinga na virusi vya corona wanapokuwa kazini.
KEMSA inatazamiwa kukadiria hasara ya shilingi billion mbili iwapo vifaa hivyo vitauzwa kwa bei ambayo imeendekezwa na wizara ya Afya.