Shule zinatazamiwa kufungwa kabla ya Ijumaa wiki hii kuruhusu maandalizi ya mitihani ya kitaifa ya darasa la nane KCPE na kidato cha nne KCSE.
Wanafunzi wa daraja la kwanza hadi tatu na wale wa darasa la tano hadi saba wanatazamiwa kukalia mitihani yao ya mwisho wa muhula kuanzia hii leo kabla ya shule kufungwa.
Wanafunzi hao kisha wataelekea kwa likizo ya mwezi Aprili ambayo itakamilika tarehe kumi mwezi wa tano wakati watarejea kwa muhula wa tatu.
Wanafunzi wa daraja la nne watalazimika kusubiri hadi mwezi Julai wakati kalenda ya masomo ya mwaka wa mwaka 2021 itangoa nanga.
Mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE unatarajiwa kungoa nanga siku ya Jumatatu huku ule wa kidato cha nne KCSE ukiratibiwa kungoa nanga Alhamisi wiki ijayo na maandalizi karibu yanakamilika.