Shirika la wakimbizi UNHCR lapinga kufungwa kwa kambi za Dadaab na Kakuma

0

Shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia wakimbizi (UNHCR) limeitaka serikali ya Kenya kusitisha mipango yake ya kufunga kambi za wakimbizi za Dadaab na Kakuma zinazotoa hifadhi kwa zaidi ya wakimbizi 500,000.

Katika taarifa, UNHCR linahoji kwamba kufunga kambi hizo kutakuwa na madhara makubwa wakati huu ambapo ulimwengu unapambana na janga la corona.

Aidha, shirika hilo ambalo limesema litaendelea kushiriki katika mazungumzo na serikali limesema Kenya inapaswa kuhakikisha kuwa limefanya maamuzi ambayo yatakuwa na suluhu la kudumu ili kuwawezesha wanaopata msaada kuendelea kupata.

Taarifa ya UNHCR inakuja saa chache baada ya waziri wa Usalama wa ndani Dr Fred Matiang’i kutoa makataa ya siku 14 kwa shirika hilo kutoa mwongozo wa kufungwa kwa kambi za wakimbizi za Dadaab na Kakuma.

Matiang’i amesema hakuna muda zaidi wa mazungumzo na shirika hilo na kutishia kuwa serikali itawarejesha wakimbizi hao makwao iwapo shirika hilo halitachukua hatua.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here