‘’Sijatangaza kwamba nataka kuwania urais na wala sijamuuliza yeyote kuniunga mkono…’
Ndio matamshi yake kinara wa chama cha ODM Raila Odinga akiwa mjini Mombasa.
Waziri huyo mkuu wa zamani akionekana kumlenga mwenzake wa Wiper Kalonzo Musyoka amesema kwa sasa kilicho muhimu kwake ni kuhakikisha kwamba mswada wa BBI umepita baada kutiwa breki na mahakama.
Odinga vile vile amesema shida kubwa inayowakumba Wakenya ni wizi wa mali ya umma huku akiwataka Wakenya kutowachagua viongozi wafisadi.
Matamshi ya Odinga kuhusu kuwania urais yanajiri siku moja baada ya Kalonzo kusema kwamba hatamuunga mkono kwa mara nyingine akisema amefanya hivyo vya kutosha.