Kinara wa ODM Raila Odinga amewasihi viongozi wa kidini kuunga mkono ripoti ya BBI.
Akizungumza katika katika eneo la Ufungamano kaunti ya Nairobi, Odinga amesema kuwa ripoti hiyo itamaliza ufisadi na ndio suluhisho kwa changamoto zinazoathiri wakenya sasa.
Tayari tume ya uchaguzi na mipaka IEBC imeidhinisha saini milioni 1.4 na sasa ripoti hio imetumwa katika mabunge yote mawili ili wajadili.