Maafisa wa Polisi wamewaonya watu wanaojaribu kutumia njia za mkato kuingia na kutoka katika kaunti za Nairobi, Nakuru, Kajiado, Machakos na Kiambu zilizofungwa.
Kamishna wa kaunti ya Nairobi James Kianda anasema watakaoruhusiwa kuingia na kutoka katika kaunti hizo ni wale walio na idhini kutoka kwa serikali ikiwemo wale waliofiwa na wapendwa wao.
Kianda anasema katika kaunti ya Nairobi, waliwashika watu zaidi ya mia moja na tisini hapo jana pekee kwa kukaidi makosa ya kuzuia msambao wa corona ikiwemo kutovalia barakoa na watafikishwa mahakamani Jumanne wiki ijayo kufunguliwa mashtaka.
Kianda amekiri kuwa hali ya sasa ni ngumu sana kwa wakenya wengi lakini akataka kila mkenya kuvumilia mradi kila mmoja asalie hai na kuonya wanaoburudika kuwa huu si wakati mwafaka.
Wakati uo huo
Wahudumu wa boda boda wameonywa dhidi ya kuwasafirisha watu kisiri katika kaunti tano zinazoripoti maambukizi mengi ya ugonjwa wa corona.
Muungano wa wanaboda boda kupitia mwenyekiti wao Kelvin Mubadi umekemea tabia hiyo ukitaja kama madharau kwa sheria.
Amewataka wana boda boda kuzingatia masharti ya usalama yaliyotangazwa na serikali badala ya kuyadharau akisema watakaoshikwa watachukuliwa hatua za kisheria.









