Vinara wa muungano wa One Kenya (OKA) wamekanusha taarifa kuwa wamekuwa wakishurutishwa kumuunga mkono kiongozi wa ODM Raila Odinga kumrithi Rais Uhuru Kenyatta.
Wakirejelea taarifa iliyochapishwa na gazeti la Nation, vinara hao Kalonzo Musyoka, Musalia Mudavadi na Moses Wetangula wametaja madai hayo kama porojo na kuvitaka vyombo vya habari kuzingatia maadili mema wanaporipoti.
Vinara hao wamedai kwamba madai hayo ni sawa na kuwashurutisha kuingia kwa muungano fulani wa kisiasa ilhali wao wamekuwa wakikutana na rais Kenyatta kushauriana kuhusu maswala yenye umuhimu wa kitaifa ikiwemo mapambano dhidi ya janga la corona.
Vigogo hao wa kisiasa wamekutana na rais Kenyatta mara mbili katika Ikulu ya Mombasa huku duru zikiarifu kuwa wanashinikizwa kumuunga mkono Odinga kwenye uchaguzi wa 2022.