Rais wa sasa wa mahakama ya Rufaa William Ouko anatazamiwa kuhojiwa kwa wadhifa wa Jaji Mkuu.
Ouko ni mzaliwa wa mwaka 1961 katika kaunti ya Siaya na aliidhinishwa kuwa wakili mwaka 1987.
Jaji huyo anahojiwa siku moja baada ya wakili Fred Ngatia kunadi sera zake mbele ya tume ya huduma za mahakama JSC ambapo aliomba asinyimwe kazi hiyo kwa sababu ya kuwa wakili wa rais Uhuru Kenyatta.
Ngatia ambaye aliwakilisha Rais Kenyatta katika kesi za kupinga ushindi wa Urais mwaka 2013 na 2017 amesema alikuwa kazini na kwamba Kenyatta kama mkenya mwingine alikuwa na haki ya kuwakilishwa.
Ngatia pia ameahidi kuhakikisha kuwa kesi zote na haswa zile za uhalifu, zinasikilizwa na kuamuliwa kwa wakati ili kuharakisha zoezi la upatikanaji wa haki.
Wengine waliohojiwa kwa wadhifa huo ni pamoja na wakili Philip Murgor, Jaji David Marete, jaji Martha Koome, msomi Profesa Kameri Mbote na jaji Juma Chitembwe.