Muungano wa ‘One Kenya Alliance’ wabuniwa

0

Viongozi wa vyama vinne vya kisiasa nchini wameungana na kubuni muungano mpya wa kisiasa unaofahamika kama ‘One Kenya Alliance’

Viongozi hao, Musalia Mudavadi wa chama cha (ANC), Moses Wetangula wa Ford Kenya, Kalonzo Musyoka wa Wiper na Gideon Moi wa (KANU) wamesema nia yao ni kuwaunganisha wakenya.

Katika kikao ambacho kilihuduriwa pia na Gavana wa Kajiado Jospeh Ole Lenku, viongozi hao wamesema vyama vyao havitakuwa na wawaniaji katika chaguzi ndogo za kaunti ya Garissa na maeneobunge ya Juja na Bonchari na badala yake kusema wataunga mkono wawaniaji wa chama cha Jubilee.

Viongozi hao pia wameapa kuandaa mikutano ya hadhara kote nchini kupigia debe mswada wa marekebisho ya katiba wa BBI pindi tu maambuki ya corona yatapungua.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here