Mwanamke ashambulia wanaume watatu na kuua mmoja Kahawa West

0

Mwanamke mmoja anayedaiwa kuwadunga kisu wanaume watatu na kisha kunywa damu yao eneo la Kahawa West amekamatwa.

Margaret Wambui Wangari anadaiwa kuwadunga kisu wanaume hao na kusababisha kifo cha mmoja wao kwa madai kuwa walikuwa wanapigana kwa sababu yake.

Mwanaume aliyefariki alidungwa kisu skioni huku wenzake wakiponea na majeraha mabaya katika tukio hilo la hapo jana katika eneo la Saa Mbaya.

Wananchi waliokuwa karibu wanaripotiwa kuingilia kati baada ya mwanamke huyo kuanza kunyonya damu ya wanaume hao.

Polisi waliokuwa wanasimamia mtihani wa darasa la nane KCPE katika shule iliyoko karibu walimwokoa Wambui kutoka kwa wakaazi waliojawa na ghadhabu ambao walitishia kumwnagamiza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here