Msajili wa vyama vya kisiasa Ann Nderitu amedhibitisha kuondoa muungano wa NASA kwenye sajili yao, kumaanisha kuwa muungano haupo tena.
Nderitu amewaandikia barua viongozi wa viliokuwa vyama tanzu vya NASA ODM, Wiper, Ford Kenya, ANC na Chama cha Mashinani kuwajulisha kuhusiana na uamuzi huo.
Hii ni baada ya ANC, Wiper na Ford Kenya kujiondoa kwenye muungano huo, wakisema kulikuwa na kutoaminiana baina yao.
Vinara wa vyama hivyo vitatu tayari wameshirikiana na kubuni muungano wa OKA ambao wanasema watatumia katika safari ya ikulu.